Maendeleo ya kiuchumi kiushirika
Kuandaa, kusimamia, kuratibu, kupanga, kuhamasisha na kukuza maendeleo ya kiuchumi kiushirika miongoni mwa wanachama wake.
Hali ya majaribio: rekodi zenye alama ya "Mfano" ni za kujaribu muundo tu, si taarifa rasmi.
Kuhusu TANCCOOPS
Madhumuni rasmi, malengo ya miaka mitano na vyanzo vya mapato vya TANCCOOPS LTD.
Madhumuni ya Mradi
Madhumuni ya TANCCOOPS LTD kama yalivyoainishwa (a)โ(k).
Madhumuni ya Mradi ni kukuza na kustawisha matakwa na hali ya kiuchumi ya wanachama kwa kupanga, kusimamia na kuboresha shughuli za maendeleo ya kilimo cha pamba na wanachama wao kwa kuzingatia misingi na matakwa ya ushirika.
Kuandaa, kusimamia, kuratibu, kupanga, kuhamasisha na kukuza maendeleo ya kiuchumi kiushirika miongoni mwa wanachama wake.
Kupokea, kuhifadhi, kuchakata na kuuza bidhaa za zao la pamba mbegu.
Kununua, kuhifadhi, kuchakata na kusambaza pembejeo na zana za kilimo kwa wahitaji, vikiwemo vyama vya ushirika na wanachama wake.
Kujipatia, kuendesha, kupangisha, kukodisha majengo na mitambo na viwanda na kumiliki ardhi.
Kumiliki magari kwa ajili ya shughuli za uchukuzi na usafirishaji wa mazao, zana na pembejeo za kilimo.
Kununua hisa na kuwekeza katika taasisi za umma, taasisi binafsi na vyombo vingine vya kiuchumi kwa idhini ya Mkutano Mkuu na ya Mrajis wa Vyama vya Ushirika.
Kutoa mikopo na misaada ya kifedha kwa wanachama wake kwa kuzingatia sheria na kanuni za Ushirika, masharti ya Mradi pamoja na miongozo ya kisheria inayoweza kutolewa mara kwa mara.
Kuendesha vituo vya majaribio ya kilimo na mashamba ya mfano na uzalishaji wa pamba na mbegu bora kwa manufaa ya vyama vya ushirika na wanachama wake pamoja na sekta ya kilimo cha pamba kwa ujumla.
Kuwa jukwaa la majadiliano, mashauriano, na maridhiano kati ya vyama vya ushirika vya pamba na wadau wengine wa tasnia ya pamba kwa ujumla.
Kuwakilisha vyama vya ushirika vya pamba katika majukwaa (Fora) kuhusiana na tasnia na biashara ya pamba kwa ujumla.
Kuwa kiungo kati ya vyama vya ushirika vya pamba na wanachama wake, serikali na wadau mbalimbali kuhusu tasnia ya pamba katika kukuza, kuendeleza na kuboresha uchumi wa wanachama na wa taifa kwa ujumla.
Malengo ya TANCCOOPS LTD kwa miaka 5
Malengo yanayopimika yaliyowekwa na TANCCOOPS LTD, kama yalivyoainishwa katika nyaraka rasmi.
200 1,000
kg / ekari
Kuongeza tija ya uzalishaji wa pamba kutoka wastani wa kilo 200 hadi kilo 1,000 kwa ekari moja, na mazao ya pamba, dengu, choroko, alizeti na mpunga kwa 250% ifikapo 2028.
+20%
Kuongeza eneo la uzalishaji wa mazao kwa 20% ifikapo 2028.
90%
Pamba daraja la kwanza
Kufikia 90% ya zao la pamba daraja la kwanza na kuongeza ubora kwa 85% kwa zao la mpunga na alizeti ifikapo 2028.
50%
Soko la mazao ya kimkakati
Kuongeza idadi na kiwango cha bidhaa katika soko ili kumiliki soko la mazao ya kimkakati kwa 50% ifikapo 2023.
1 12
watendaji
Kuimarisha ufanisi wa utendaji katika chama kwa kuongeza watendaji kutoka 1 hadi 12 ifikapo 2028.
Kuongeza vyanzo vya mapato ya Mradi ifikapo 2028.
Takwimu na tarehe zimehifadhiwa kama zilivyo katika nyaraka rasmi.
Vyanzo vya mapato ya TANCCOOPS LTD vitatokana na:
Biashara na shughuli zinazoiwezesha TANCCOOPS LTD kujiendesha kwa uendelevu.
Kama vile ushuru wa usindikaji, mauzo ya pembejeo na kamisheni katika usambazaji wa vifungashio.
Kutoka benki, asasi nyingine za fedha na mifuko ya hifadhi ya jamii.
Kutoka taasisi na asasi nyingine.
Kwa ajili ya kufanyiwa biashara kama ilivyo katika masharti ya Chama.
Viingilio, ada, mauzo ya masharti, vitabu, vitambulisho, fomu mbalimbali na michango maalum kutoka kwa wanachama.
Chanzo: nyaraka rasmi za TANCCOOPS LTD.