Dira
“Kuwa na Ushirika wenye wanachama walio na nguvu kiuchumi kutokana na fursa za kilimo na maliasili zilizopo ndani ya Mikoa inayozalisha Pamba.”
Hali ya majaribio: rekodi zenye alama ya "Mfano" ni za kujaribu muundo tu, si taarifa rasmi.
Tanzania Cotton Co-operatives Joint Enterprise Limited
TANCCOOPS LTD ni mradi wa pamoja wa Vyama Vikuu vya Ushirika 13 vinavyojishughulisha na zao la pamba, vikiunganisha nguvu katika mikoa minane (8) ya Tanzania Bara.
Mambo muhimu
Sisi ni nani
Tanzania Cotton Cooperative Joint Enterprise (TANCCOOPS LTD) ni mradi wa pamoja wa Vyama Vikuu vya Ushirika vinavyojishughulisha na zao la pamba nchini Tanzania.
TANCCOOPS LTD ilianzishwa na kusajiliwa rasmi kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya mwaka 2013, tarehe 26 Februari 2020, ikiwa na Namba ya Usajili AFF-SHY-SHY-MC-2023-100. Makao makuu ya TANCCOOPS LTD yapo mkoani Shinyanga, huku wanachama wake wakiwa katika mikoa minane (8) ya Tanzania Bara.
Hadi sasa, TANCCOOPS LTD ina wanachama 13, ambao wote ni Vyama Vikuu vya Ushirika vinavyohusika na zao la pamba nchini Tanzania.
Kuhusu TANCCOOPS
Mwelekeo wetu
“Kuwa na Ushirika wenye wanachama walio na nguvu kiuchumi kutokana na fursa za kilimo na maliasili zilizopo ndani ya Mikoa inayozalisha Pamba.”
“Kuwezesha shughuli za vyama wanachama kwa kutoa huduma bora za kukusanya, kusindika, kuuza bidhaa za kilimo na maliasili, kutoa ushauri elekezi na kutoa taarifa sahihi na kwa wakati kwa wanachama na wadau.”
Iwe wewe ni chama mwanachama, mdau wa serikali, mwekezaji au mbia wa maendeleo — tuko tayari kushirikiana nawe.